SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 12 Machi 2018

T media news

Simba Kuondoka Jumatano Kwenda Misri kwa Mchezo wa Marudiano

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC, Jumatano ya wiki hii.

Simba itaondoka Jumatano hii ya Machi 14 2018 ikiwa na kumbukumbu za kulazimishwa sare ya mabao 2-2 kwa mawili, hivyo itakuwa na kibarua kigumu ugenini.

Matokeo iliyoyapata Simba awali, sasa inapaswa kwenda kupata ushindi wa bao moja bila majibu ama zaidi ya hilo moja ili kujiwekea nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Bocco na Okwi ndiyo walikuwa wafungaji wa mabao ya Simba yaliyofungwa kwa njia ya adhabu ya penati.

Mechi hii ya marudiano itapigwa Jumamosi ya wiki hii, Machi 17 2018 kwenye Uwanja wa Port Said huko Misri.