SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 12 Machi 2018

T media news

Naibu Katibu Mkuu wa Bavicha Ajiuzulu Wadhifa Wake

Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Gertrude Ndibalema amejiuzulu wadhifa huo kuanzia jana Machi 11,2018.

Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 ametangaza kujiuzulu kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsi.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 12,2018 Gertrude amesema, “Ni kweli nimeamua kuachia nafasi yangu ili kutimiza malengo ya shughuli zangu binafsi.”

“Kwa kuwa nakipenda chama changu na kwa taaluma yangu (mawasiliano kwa umma) ili kuepuka mgongano, nimeamua kukaa pembeni ili kutimiza azma yangu na nitabaki kuwa mwanachama,” amesema.

Gertrude ni kiongozi wa pili wa ngazi ya juu Bavicha kujizulu akitanguliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi aliyejiunga na CCM.