SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 14 Machi 2018

T media news

Mourinho “Ni Kocha Mbovu Katika Historia ya EPL”

Manchester, England
Kocha mkuu wa Man United amejibu wa vijembe ambavyo vililengwa na aliyekuwa kocha wa Crystals Palace Bwana Frank De Boer. De Boer alisema Rashford ni mchezaji mzuri lakini hapaswi kucheza chini ya Jose Mourinho. Kauli hii imekuja baada ya rashford kufanya vizuri kwenye mchezo wake dhidi ya Liverpool Ugani Old Trafford kwa kudumbukiza kamba mbili.

Jose Mourinho nae hakukaa kimya baada ya kusema kuwa hawezi kujibizana na kocha mbovu kuwahi kutokea katika historia ya Ligi kuu England. De Boer alifukuuzwa Crystals Palace mwezi wa 9 mwaka jana baada ya matokeo mabovu. Alifanikiwa kuiongoza Palace kwenye michezo mitano na siku 77 kama meneja wa Palace. Matokeo mabovu ya kufungwa michezo minne kati ya mitano iliwatia wasiwasi mkubwa sana uongozi wa Palace hali iliyofanya kumtimua.

Kauli ya Mourinho imekuja baada ya kuulizwa kuhusu uwezekano wa Rashford kuanza kwenye mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Seville.

akasema “nimeona baadhi ya komenti kutoka kwa kocha mbovu kuwahi kutokea katika ardhi ya waingereza akiongelea wachezaji wangu, anachokisema huyo kocha hata simuelewi, anadai kuwa Rashford hapaswi kufundishwa na kocha kama mimi? Mimi nachoangalia ni ushindi tu sio vingine, kama Rashford angefundishwa na yeye angekuwa amejifunza kufungwa tu maana hakuna kitu De boer anachojivunia zaidi ya kupoteza mechi ovyo”

“wanasema kuwa simpi kijana nafasi, nadhani hao wanaosema hivyo hawajielewi, ukijaribu kuangalia takwimu, Rashdord ni moja kati ya wachezaji watano waliocheza michezo mingi zaidi Man United,. Sasa unasemaje simpi nafasi? Kikubwa alichohitaji Rashford ni nafasi ya kucheza basi, mimi sifundi mtu namna ya kucheza, nachompa ni nafasi ya kupata uzoefu mengine ni jitihada za mchezaji.”

Kauli hizi zimeambatana pia na maneno yaliyotolewa na Garry Neville lakini Mourinho aliona asimwache De Boer hivi hivi. De Boer anasema nafasi ambayo Rashford anayopewa ni finyu, na mara nyingi amebanwa na mbinu za mourinho ambazo zinalenga zaidi kupata matokeo bila kuangalia namna ya kukuza vipaji vya vijana wadogo.

United Inajianda kukutana na Sevila katika mchezo wa marudiano ugani Old Trafford baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya bila kufungana. Man United haijawahi kupoteza mchezo wowote nyumbani kwenye michuano ya UEFA tokea mwaka 2013 walipofungwa na Real Madrid.

Michael Owen alishagazwa sana na matokeo yale kwa kuai ni aibu kwa Man United kufunga magoli 7 kwenye michezo 15 dhidi ya Vilabu vya Hispania. Ila Michael Owen bado anaamini Ol Trafford ni mlima mkubwa sana maana Man United imeruhusu magoli machache sana kwenye michuano ya uefa hivyo hategemei Sevilla kupata magoli mengi. Matokeo ya awali yalipondwa sana na mchezaji wa zamani wa Man United Roy Keane.

Kauli za Roy keane zimekebehi aina ya uchezaji wa Man United kwa kudai kuwa hakukuwa na haja ya Kikosi cha Man United kuhangaika kumkaba Ever Banega kana kwamba wanamkaba Messi au Ronaldo.

Amesema kwa sasa United inemtegemea De Gea ni aibu kubwa kwa tinmu kubwa kama hii kuishi kwa kudra za Golikipa huku miguu ya washambuliaji ikiwa na kigugumizi. Anaamini kuwa lawama nyingi ziwaendee Sanchez na Lukaku ambao wameshindwa kabisa kupenya lango la wapinzani na anaamini kuwa watakuwa na deni kubwa sana mbele ya mashabiki kwenye mchezo wa hivi leo. Hofu kubwa ipo kwa Anthonio Martial, Paul Pogba, pamoja na Ander Herrera ambao wote haijulikani kama wataanza au lah.