SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 11 Machi 2018

T media news

Mapya Yaibuka..Emmanuel Mbasha Amwangukia Flora Mbasha

MWIMBAJI wa injili Emmanuel Mbasha amefunguka na kumshukuru aliyekuwa mkewe, Madam Flora kwa kumzalia mtoto wa kike mzuri huku akilalama kwa kunyimwa fursa ya kuonana na mwanaye huyo kwa muda wa miaka miwili sasa.

Mbasha kupitia Instagram amefikisha kilio chake kwa mzazi mwenzake huyo ambaye sasa ameolewa na Daudi Kusekwa na kumtaka japo kumpa haki ya kuonana na mtoto wake huyo ambaye anadai kuwa amemlea tangu akiwa mdogo.

 “Ulinizalia mtoto mzuri sana kwa hilo nakushukuru mno. Nimemmiss Lizy sana unipe basi mtoto unaninyima kabisa daah karibu mwaka wa pili inaelekea wa tatu sasa sijamwona mtoto. Du, mimi baba yake tu ila nakuomba hata siku moja moja nifurahie maisha na dogo basi nakuomba nimwone mwanangu Lizy.


“Najua hata mtoto amenimiss sana, kwa mana ameondoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tangu mtoto ila anashindwa kuongea tu, najua ananikumbuka sana.” 


“Mahakama iliamua mtoto akae na Mama ila niwe namwona, sasa unapingana na mahakama. Sitaki povu nimeongea na mzazi mwenzangu X wife, mke wa mtu.. njia za kawaida naona imeshindikana unakaza sana aise sasa inabidi nikuombe Insta tu,” alisema Mbasha