SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 10 Februari 2018

T media news

Mtulia: Polisi Msiwafanye Waendesha Bodaboda Kama Gari Lenu la Mshahara

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amelitaka Jeshi la Polisi hasa wa usalama barabarani waache kuwafanya waendesha bodaboda kama gari lao la mshahara kwa kuwabambikia kesi zisizokuwa za kweli pindi wanapo wakamata.

Mgombea huyo ametoa kauli hiyo akiwa kwenye muendelezo wa kuomba ridhaa huku zikiwa zimebakia takribani siku saba ili wananchi wa Jimbo la Kinondoni pamoja na Siha kushiriki zoezi la kupiga kura katika uchaguzi huo mdogo wa marudio na waweze kupata wawakilishi wao ambao kwa mara ya kwanza wataingia bungeni mjini Dodoma Aprili 03 endapo zoezi hilo litakamilika kwa amani na usalama.

"Tuna kwenda kuhakikisha tunaleta mfumo mzuri wa kuvitambua vituo vyote vya bodaboda pamoja na kuvisajili ndani ya Jimbo la Kinondoni lakini tunawambia polisi hawa vijana wamejiajiri wasibuguziwe, sio watuhumiwa wala majambazi", amesema Mtulia.

Pamoja na hayo, Mtulia ameendelea kwa kusema "naenda kupiga marufuku bodaboda kuwa gari la mshahara kwa polisi, wakamateni wanapokuwa na makosa ya kisheria na wala msibawabikize kesi".

Kwa upande mwingine, Mtulia amedai endapo atarudishwa na wananchi hao katika Jimbo la Kinondoni basi atahakikisha matatizo yote waliyokuwa nayo yatatatuliwa bila ya wasi wasi wa aina yeyote.