SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 10 Februari 2018

T media news

Temba Afunguka Kuhusu Kumfumania Mkewe na Mwanaume Mwingine

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka kundi la TMK Wanaume na kiongozi wa Mkubwa na Wanaye Mhe. Temba anadaiwa kumfumania mkewe akiwa na mwanaume na ndiyo chanzo cha kuachana na mkewe huyo Bibi Cheka ameweka wazi.

Akiongea kwenye kipindi cha eNewz Bibi Cheka amesema kuwa Mhe. Temba alimfumania mkewe akiwa na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake na kumfukuza kisha mwanamke huyo kuolewa na mwanaume mwingine, Bibi Cheka amemwaga mchele huo baada ya kusikia Temba akijitapa kuwa uongozi wao ulimmjengea nyumba kubwa na kudai kuwa bibi huyo hana shukrani.

Kwa upande wa Temba alifunguka na kusema kuwa hizo taarifa hazina ukweli wowote kwani yeye na familia yake wapo vizuri wala hakuna jambo kama hilo analodai Bibi Cheka

"Hapana mimi nipo na familia yangu watoto zangu wapo nyumbani na mama yao yupo likizo saizi hivyo nimetoka hapo ameniandali chai vizuri saizi ndiyo natoka kwenda kuonana na jamaa zangu tunakikao kidogo , sasa sijui yeye anaushahidi gani kusema nimeachana na mke wangu na hata kama kweli labda nimeachana naye haihusiani na mambo haya tuzungumze mambo ya muziki, sijawahi kumfumania mke wangu na sijui kwanini bibi amezungumza hayo huenda labda amekasirika"