SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 14 Februari 2018

T media news

Inachokifanya Mahakama Kuu mkoa wa Mara na Kigoma kuhusu huduma za kisheria

Leo February 14, 2018 Moja ya stori niliyoipata ni kuhusu uboreshaji wa huduma za Mahakama ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania imeanza ujenzi wa Mahakama Kuu mbili katika mikoa ya Mara na Kigoma ili kuwasaidia wananchi wasitembee umbali mrefu kutafuta huduma za kisheria.

Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Zilliper Geke amesema kuwa ujenzi wa mahakama hizo umeleta faraja na ukumbozi kwa wananchi wa mikoa hiyo.

Amesema wananchi wa mkoa wa Mara wamekuwa wakisafiri imbali wa Kilometer 218 kwa ajili ya kwenda Mahakama Kuu ya Mwanza ili kufata haki yao.

“Kwa kweli wananchi wà mkuo huu wamefarijika sana, hivyo kukamilika kwa mradi huu utawaondolea usumbufu wa kusafiri hadi kuelekea Mwanza,”-Zilliper

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi, Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi amesema kuwa ujenzi wa Mahakama Kuu Musoma ambao unasimamiwa na ‘HAB Consult’ na ‘Mbega Associates’ unaenda sambasamba na Ujenzi wa Mahakama Kuu Kigoma