Leo Rais Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa. Akiwa katika kitanda cha hospitali amemwambia Rais Magufuli kuwa CCM ni chama chake na amekiunda yeye.
“CCM ni chama changu nimetoka tu, tumeachana lakini nimefanya kazi zote, nimekiunda mimi, hakiwezi kuwa kinyume changu,”– Mzee Kingunge
==>Msikilize Hapo Chini