SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 5 Januari 2018

T media news

Tunda: Nipo Tayari Kuwa Mke wa Mtu

MUUZA nyago aliyejizolea umaarufu kutokana na vituko vyake, Tunda Sebastian, amefungukia kubadili muonekano wake kuwa, amefanya hivyo ili kukwepa kuonekana na mwili wa kitoto tena.

Akizungumza na Star Mix,Tunda alisema kuwa anapendezwa na muonekano ambao anaonekana hivi sasa kwa sababu angalau anaonekana mtu mzima hata mtu akimuoa anajua ana mke mkweli ndani.

“Nafurahia sana muonekano wangu wa sasa hivi nilivyo na kwa sasa nipo tayari kuitwa mke wa mtu maana hata nikiwekwa ndani kama mke nafaa kabisa, nilikuwa nakereka watu kunifananisha na katoto,” alisema Tunda.