SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 5 Januari 2018

T media news

Nini kitatokea kwa fedha zako endapo benki inayozitunza itafungwa?

Majengo Pacha ya Benki Kuu ya Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina), Dar es Salaam

Benki ni sehemu salama zaidi ya kutunza fedha zako. Hata hivyo zipo nyakati ambazo benki hufilisika. Benki inapofilisika, fedha zako kuna uwezekano mkubwa kwamba ziko salama. Nchini Tanzania benki na taasisi zote za fedha zinatakiwa kisheria chini ya Benki Kuu ya Tanzania, kuwa wanachama wa Bodi ya Bima za Amana (Deposit Insurance Board), kwa hiyo kwa kuwa benki na taasisi zote za fedha lazima kisheria ziwe wanachama wa bodi hii, benki au taasisi inapofeli basi huna haja ya kupata wasiwasi.

Benki hufeli na kufilisika pale zinaposhindwa kutimiza majukumu yake ya kibenki. Mfano wakati Benki Kuu ya Tanzania ilipotangaza kuzifuta baadhi ya benki mapema mwezi Januari 2018 kama Efatha, iliweka bayana kwamba benki hizi zimeshindwa, pamoja na mambo mengine, kulipa madeni yake na kuishiwa na mtaji.

Benki haziweki fedha zako katika sefu, bali inazifanyia biashara kupitia uwekezaji kwa riba. Benki zinaweza kupoteza fedha nyingi kupitia uwekezaji, au zinaweza kushindwa kukupa fedha pale  unapokwenda benki kutoa. Kadiri benki zinavyopata hasara katika ukopeshaji wake ndiyo uwezekano wa kufilisika unavyoongezeka.

Nani analinda fedha zako iwapo benki inafilisika?

Benki Kuu ya Tanzania kwa niaba ya serikali, ina jukumu la kulinda fedha za wateja iwapo benki inaingia matatizoni. Sheria ya Fedha ya mwaka 2006 imeipa jukumu Benki Kuu ya Tanzania kuwa na Bodi ya Bima ya Amana ambayo ndiyo yenye jukumu hilo.

Katika hili, majukumu ya bodi hiyo katika fedha iliyopo benki ni:

a) Kufanya malipo ya shilingi 1,500,000 baada ya kutoa madeni ambayo mteja anadaiwa na benki au taasisi ya kifedha iliyofilisika. Awali kiwangi hiki kilikuwa shilingi 500,000.

b) Kupokea malalamiko. Inapotokea benki ikafilisika mteja anapaswa kupeleka lalamiko katika bodi hii kabla ya kulipwa.

c) Kuitisha na kuhakiki vielelezo. Kabla ya kulipwa, mteja anapaswa kuwa na vielelezo vyote ambavyo bodi itahitaji ili kujiridhisha ustahiki wake wa malipo husika.

Soma zaidi kuhusu Bodi hiyo ya Benki Kuu katika tovuti ya BoT hapa.

Ziada:

Ukiwa na fedha nyingi zaidi ya shilingi milioni 1.5, unapewa kwanza malipo ya awali ya shilingi milioni 1.5, kisha unasubiri malipo mengine baada ya hatua ya “Liquidation”. Hatua hii hufanyika kwa kufuata makundi, wanaanza kulipwa wenye ubia wa mtaji wa benki na makundi mengine ambayo yanaidai benki. Mfano benki itapiga mnada majengo yake, vitu vya thamani na kadhalika na kulipa wanaoidai, ikiwemo wewe mteja mwenye fedha ya ziada. Zoezi zote hili wakati huo linakuwa chini ya serikali.

Kwenye utaratibu wa kulipa madeni, wateja wenye amana kama wewe huwa ni wa awali kabisa, wenye ubia benki (shares) huwa ni wa mwisho, na kama ni hasara wabia hugawana hiyo hasara kama ambavyo hugawana faida.

Jambo muhimu zaidi ni wateja kusoma taarifa za fedha za benki zao kila kota, kwani ni jukumu lao ili kufahamu mwenendo wa benki mara kwa mara.

Ndeyanka Mushi

Follow me on Twitter & DM.