Mbunge wa Mbeya Mjini na Mkongwe wa Hip Hop, Joseph Mbilinyi 'Sugu'amesema kwamba muziki wa zamani umepitia changamoto nyingi sana ndiyo maana hata katika mistari ya Albam zake za mwanzoni kulikuwa na manenoo ya kiharakati sana.
Akisikika kwenye Planet Bongo Radio, Sugu amesema wakati wakifanya muziki wa zamani changamoto za mitaani walikuwa wakiiweka kwenye nyimbo ikiwa hata purukushani za maaskari na vijana wa mtaa lakini kwa sasa hawezi kuimba vile kwa kuwa ataitwa mchochezi.
Sugu ambaye aliingia Bungeni 2010 amesema kwamba pamoja na kwamba muziki wa zamani haukuwa na kelele za mitandao au picha za utupu, ukweli ndiyo ulikuwa silaha kubwa kwa msanii ili mtaa uweze kumuelewa.
"Love ya mtaa ni kila kitu. Ukishakubalika mtaani hata wa ushuani lazima akubali. Nilikuwa nafanya vitu real, kuwa mkweli kwa watu wangu kulinifanya ni kiki hayo mambo mengine sisi tulikuwa hatuna zaidi ya 'Street Credibility" Sugu.
Sugu anatajwa kama moja ya wasanii wachache wlioweza kubadilisha misimamo ya wazazi wengi na kuamini muziki wa kizazi kipya siyo uhuni.