SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 5 Januari 2018

T media news

Mke wa Kingunge afariki, Kingunge alazwa hospitali

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale mwiru, Peras kingunge a,efariki dunia jana Alhamisi, Januari 4, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu.

Afisa Mahusiano ya Umma wa hospitali ya Taifa Muhimbili, John Stephen ameeleza kuwa Mama kingunge alifariki jana, Alhamisi, majira ya saa 8 mchana katika wodi ya sewahaji alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Stephen alisema kuwa, mke wa mwanasiasa huyo mkongwe, alilazwa hospitalini hapo tangu Oktoba 3, mwaka jana.

Aliongeza kuwa wakati Mama Peras anafariki, Mumewe, Mzee Kingunge naye alikuwepo hospitalini hapo akipatiwa matibabu.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mama yake, na kueleza kuwa kimetokea wakati ambapo baba yake pia ni mgonjwa.

“Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling’atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka,” amesema Kinje.