Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
05/01/2018
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda* , Leo amehaidi Kuijengea Nyumba ya Vyumba Vinnie (4) Familia ya Mwandishi (mpiga picha) wa Magazeti ya Serikali TSN wanaochapisha Magazeti ya Habari Leo na Daily News Marehemu *Athumani Hamis* ambae amezikwa Leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Ahadi hiyo Imetolewa na *Mkurugenzi Mtendaji wa TSN Dkt. Yonaz* kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe Paul Makonda* ambae aliombwa kuisadia familia ya Marehemu ambayo ina watoto Wanne wanaosoma uku wakiwa wanaishia kwenye Nyumba ya kupanga kutokana na Baba yao kuugua kwa zaidi ya Miaka 10 na hivyo kushindwa kufanya kazi.
*Dkt. Yonaz* amesema Mhe Makonda kwa kutambua mchango wa tasnia ya Habari hususani *waandishi wa Habari* amekubali kujenga Nyumba hiyo kama kielelezo cha Kumuenzi *Marehemu Athumani* ambae katika Uhai wake alikuwa Mpiga Picha Mahiri wa Magazeti ya Serikali nchini.
*Hatua* hii imepokelewa kwa *Furaha* na baadhi ya waandishi wa Habari ambao wamesema Kitendo cha Makonda kukubali Kuijengea *Nyumba* Familia ya Marehemu Athumani mbali na kuwafuta Machozi ya Huzuni, Bali kimekuwa ni fundisho Tosha kwa Baadhi ya waandishi ambao walikuwa Wakimchukia *Mhe Paul Makonda* pasipo sababu za Msingi, na kukifananisha Kitendo hiki na Ukamilifu wa Maandiko katika vitababu vitakatifu yanayotutaka *TUWAPENDE ADUI ZETU.*