SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 7 Desemba 2017

T media news

SALAM ZA KARIBU KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU UVCCM TAIFA. KUTOKA KWA MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA NA MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA NDUGU


Mohamed Awadh.

Ndugu wajumbe wa mkutano mkuu UVCCM TAifa karibuni sana Mkoani dodoma, natambua mmejiandaa vya kutosha kuja kushiriki nasi zoezi la kumpata mwkt wa jumuiya yetu kwa Ngazi ya Taifa atakaye tuongoza kwa miaka mitano. Kwa kuwa tunahitaji kuihuisha nguvu na mchango mkubwa wa UVCCM katika kujenga zaidi umaarufu na mapenzi ya wananchi kwa CCM, BINAFSI niliwachukua wagombea wote na kuwachambua pia kujiuliza maswali kadhaa juu ya aina gani ya mwkt kama jumuiya tunamuhitaji. Ndipo nikagudua kwa wakati wa sasa si Mwingine ila ni *Kheri James* pekeee ndie anaye weza kutuvusha na kuiimarisha jumuia yetu kwa heshima kuu na unyenyekevu wa hali ya juuu Nawaombeni vijana wenzangu na wajumbe wa mkutano mkuuu UVCCM Tumuunge mkono na kumchagua KHERI JAMES

*TUNAMCHAGUA KHERI JAMES KWA KUWA ANASIFA ZIFUATAZO* :

1.Kheri james ni kijana Mwenye uwezo mkubwa kisiasa wa kuhamasisha wananchi kuipenda CCM, jumuia zake na SERIKALI. Nikijana Anayeweza kwa mfano kuwasisimua watu milioni moja katika Mkutano wa Hadhara akasababisha nderemo, vifijo, shangwe na mbinja zinazo shinikiza mbingu  kuonesha raha na upendo wa hadhara kwa CCM na Serikali.

2. Kheri James ni kiongozi Mwenye ufahamu mkubwa wa Chimbuko la CCM, Jumuia zake, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya kutetea na kulinda misingi ya Chama na jumuia zake na kutetea na kuulinda  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mjuzi na mweledi wa Dira ya Nchi, Sera, Sheria, Kanuni, Malengo, mikakati ilivyo kwenye ilani ya uchaguzi kama inavyotekelezwa chini ya Katiba ya Chama na  Katiba ya Nchi. *Ukitaka kuthibitisha hili unaweza kuangalia YOUTUBE MDAHALO WAKE WA MWAKA 2014 Star Tv usiku*.

3. Pia kheri James ni kiongozi Mwenye UTU wa kuguswa na mahangaiko na Shida zinazowakabili atakaowaongoza kwa kuwahurumia na hivyo kuonesha moyo wa kuwasaidia kwa kadri ya uwezo wake ikiwemo kupigania HAKI zao za msingi.aliyafanya hayo alipokua mwkt wilaya ya ilemela.

4. Kheri James pia ni Mwenye ujasiri na kujiamini katika kufanya maamuzi yenye faida kwa wengi, uwezo wa kukemea MAOVU katika jamii, uwezo wa kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya vikao na utayari wa kupokea LAWAMA inapobidi.ukiangalia warsha na makongamano aliyopewa nafasi ya kuzungumza ndani ya chama na nje ya chama hakuacha kujipambanua katika haya.

5. Pia kheri James ni kiongozi Mwenye uwezo mkubwa wa kusikiliza, kuwa tayari kukosolewa na kuonesha uvumilivu wa kiasi cha wastani dhidi ya wakosoaji wasio na lugha za staha.

6. Mbali na hayo kheri james ni kiongozi Anayejishusha na kujumuika kirahisi katika makundi anuai katika jamii bila kujali tofauti za kikabila, kidini, eneo atokako mtu au makundi ya kisiasa ndani na nje ya Chama.tumeyaona haya akiyaishi kwa vitendo ndani ya jumuiya yetu ya vijana na sisi tunahitaji mtu wa namna hiiii anayetokana na sisi.

7. Lakini pia ndugu zangu *kheri James* ni kiongozi Anayetoa ahadi ambazo ZINATEKELEZEKA kwa uhalisia wake.hata alipo pita kwenye wilaya na mikoa yetu ninyi nimashahidi. Huyu tusimuache anatufaa nikheri pekee.

8. Pia ndugu *kheri james* ni kiongozi kijana Mwenye uwezo wa kuhimili makabiliano ya kisiasa dhidi ya wapinzani wake ndani na nje ya chama bila jazba wala kutumia  lugha zinazochafua taswira nzuri ya Chama kwa umma. Tafsiri hapo ni mgombea Anayejiheshimu na kuheshimu wengine. Ndugu zangu mkitaka kuamini haya chama kilipitia kipindi kigum sana 2013-14 mpaka 2015 kipindi mh Nape Mnauye akiwa na dhama ya itikadi na uenezi aliwahi pata mualiko wa mdaharo lkn ikatokea dharula aliye ifuta aibu ile ambayo chama chetu ingeingia ni *kheri James* pekeee video mitandaonih zipo mnaweza kujiridhisha.

Ndugu wajumbe wa mkutano mkuuu Uvccm Taifa wakati mnapo jiandaa kuja dodoma niwaombe muendelee kufikiri juu ya busara ya kumchagua ndugu Kheri James ili aje kuwa mwkt wetu ili atuvushe salama kipindi hiki kigumu cha reformationna transformation ambayo chama na jumuiya zake inapitia ili kujiimarisha Zaidi. *HAKIKA TUKIENDA NA KHERI JAMES ITAPENDEZA ZAIDI. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. NA KARIBUNI DODOMA*

NA
*Mjumbe wa mkutano mkuu CCM TAIFA ndugu Mohamed Awadh*.
Email. Mohamedkeref2@gmail.com
0719969023/0762890656.