Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa aliwapa Takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka kuhusu tuhuma za kununuliwa kwa baadhi ya madiwani wa Chadema na kuhamia Chama cha Mapinduzi(CCM) huku akihoji kuwa tuhuma na ushahidi wa rushwa ukiletwa na mwanasiasa rushwa inabadilika rangi?.
Mh. Nassari ametumia ukurasa wake wa Instagram kuyaeleza hayo huku akisema kuwa aliwapa Takukuru moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa.
“Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka”
niliwapa takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa. Na wakasema wana teknolojia ya hali ya juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo.
Cha ajabu hawajaona UHALISIA au UONGO uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi. TAKUKURU wanasema iliingizwa siasa, swala la kujiuliza, “Hivi kumbe tuhuma na ushahidi wa rushwa ukiletwa na mwanasiasa rushwa inabadilika rangi”?
Hivi karibuni kuliibuka na tuhuma kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa(Takukuru) kuwa wamefuta ushahidi wa Mbunge huyo kwa kile kilichodaiwa kuwa wameharibu uchunguzi wa chombo hicho kwa kueleza kila kwa vyombo vya