SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 1 Desemba 2017

T media news

Mbunge Prof. Jay Aangua Kilio Hadharani, Baada ya Mauaji yaliyofanywa na Polisi Jimboni Kwake

Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ameangua kilio hadharani kwenye mkutano aliokuwa amefanya na wananchi wa kijiji cha Ruhembe wilayani Kilosa na kuwaomba Waziri wa mambo ya ndani na waziri mkuu wachukue hatua kabla ya wananchi kujichukulia hatua

Wananchi hao pia waligoma kuzika mwili wa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Salim Said Mheka mwenye umri wa miaka 17 aliyeuawa na polisi wa kitengo maalumu kwa madai kuwa alikuwa ni mhalifu wa Kibiti

Kijana huyo alimaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari Ruhembe,

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro amesema kijana huyo alikuwa anajihusisha na ugaidi

VIDEO: