Katibu wa Itikadi na uenezi taifa wa chama cha mapinduzi CCM Bwana Haphrey Polepole ambae alikuwa Mgeni rasmi na msimamizi mkuu wa uchaguzi wa kuwapata viongozi ngazi ya mkoa na uwakilishi taifa amegongelea msimali kwa wanachama wanaotaka kujiunga na CCM kwa kuwataka kufuata utaratibu uliowekwa katika katiba ya chama hicho na siyo kujiondokea mtandaoni na kurudia mtandaoni.
Amesema kuwa kwa sasa CCM ni chama chenye thamani kwakuwa kinatekeleza yale yaliyoandika katika ilani yake ya uchaguzi na kimeanza kuonyesha imani kwa wengi na ndio maana watu wengi wanajiunga nacho hivyo siyo kila anaetaka kujiunga anaweza kuruhusiwa kirahisi lazima ajadiliwe kupitia vikao mbalimbali na inabidi aombe kupitia tawi la Mtaa anaotokea.