SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Novemba 2017

T media news

Waliozama ziwa Victoria waokolewa

Watu 17 wamenusurika kifo baada ya meli ya MV Julius waliyokuwa wakisafiria kuzama jana usiku ndani ya ziwa Victoria kilomita chache kutoka kisiwa cha Goziba wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera.

Meli hiyo ya mizigo ilipinduka na kuzama muda mfupi bada ya kuondoka katika kisiwa cha Goziba, wilayani Muleba mkoani Kagera ikielekea Mwanza usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa majeruhi wote waliookolewa wako salama.

“Habari za awali zinaeleza kwamba hao wote waliokolewa katika hilo tukio, lakini pia maafisa wangu wako eneo la tukio wakiwepo wanamaji kutoka Kagera waliiondoka alfajiri kwa ajili ya kwenda kuangalia na kuhakikisha kama kuna dalili yoyote ya mtu aliyesahaulika,” alisema Kamanda Ollomi.

Mmiliki wa meli ya MV Julius, ameeleza kuwa alipata taarifa kuwa meli yake ilipata hitilafu muda mfupi baada ya kuondoka kisiwani hapo lakini pamioja na jitihada zilizofanyika hazikufua dafu jambo ambalo lilipelekea kuzama kwa meli hiyo.