Watu 11, abiria 10 na rubani wamefariki dunia kufuatia ajali ya ndege ya Shirika la Coastal Aviation, iliyoanguka katika eneo la kreta ya Empakaai, ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 7 mchana ambapo imeelezwa kuwa kutokana na hali mbaya ya hewa ndege hiyo ilijigonga katika kingo za milima ya kreta hiyo na kuanguka.
Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Kilimanjaro kuelekea Seronera Serengeti.
Hizi hapa ni baadhi ya picha za mabaki ya ndege hiyo iliyoanguka.
Mabaki ya Ndege ya Shirika la Coastal Aviation iliyoanguka eneo la kreta ya Empakaai, ndani ya hufadhi ya Ngorongoro.
Wananchi wakishangaa mabaki ya Ndege ya Shirika la Coastal Aviation iliyoanguka eneo la kreta ya Empakaai, ndani ya hufadhi ya Ngorongoro.
Wananchi wakishirikiana na Polisi kuiweka vizuri miili ya waliofariki katika ajali ya Ndege ya Shirika la Coastal Aviation iliyoanguka eneo la kreta ya Empakaai, ndani ya hufadhi ya Ngorongoro.