"Wanandoa wawili Bi Ester na mume wake Bw Jonathan waliokuwa wakipendana sana waliishi miaka mitano ndani ya ndoa yao kwa amani sana, miaka yote hiyo walikuwa wanapendana sana, japokuwa kukwaruzana ndani ya mahusiano ni jambo la kawaida lakini walihakikisha wanayamaliza mambo yao kimyakimya ili kutowapa faida watu wa nje, Miaka ilizidi kukatika, hatimae bi Ester akabeba ujauzito, Bahati mbaya baada ya ujauzito ule kufikisha miezi minne tu mumewe Jonathan aliugua sana ugonjwa wa ajabu, kwani alikuwa akianguka ovyo na kuanza kukimbia peke yake, hakuwa na tofauti na mwehu muda huo, uzuri Jonathan alikuwa na ndugu wengi ambao baada ya kupata taarifa kuwa ndugu yao ameugua walijazana kwa wingi nyumbani kwa Jonathan,, Wakati huo wote bi Ester alikuwa akimuuguza mumewe na kupambambana na misukosuko ya hapa na pale, alikubali hata kumshikilia mumewe asiweze kukimbia kwani alionekana kichaa kabisa muda huo, hakujali hata kama alikuwa na mimba ambayo ilikuwa inahitaji matunzo pia ila alipambana kuhakikisha mumewe Bw Jonathn anapona..
************************
"Hadi ndugu zake na Jonathan wanakusanyika, bi Ester alikuwa ameshaleta daktari aliyekuwa anamtibu Jonathan palepale nyumbani, kwa kuwa Mungu aliwajaalia uwezo wa mali swala la kumuuguza mumewe halikuwa gumu sana, hakujali kama mali zitaisha alichojali muda huo ni kuhakikisha anapambana na mauti yaliyokuwa mbele ya mumewe labda mungu mwenyewe atamchukue ila siyo kifo kisababishwe na ukosefu wa mali, Alidiliki hata kugombana na ndugu zake na Jonathan walipojaribu kumgombeza kuwa anaharibu mali kwa ajili ya matibabu ya mumewe, haya ni baadhi ya maneno aliyoongea kaka yake na Jonathan akimwambia Ester nanukuu kidogo
"SHEM, HIZO PESA UNAZOTUPA KUMTIBU MUMEO SI UZIACHE TU ILI ZISAIDIE MSIBANI, MDOGO WANGU HAWEZI KUPONA NA NAKUONA KABISA UNAVYOZITOLEA MACHO MALI ZAKE"
Bi Ester hakujibu kitu zaidi ya kusimama na kwenda kumuinua mumewe aliyekuwa chini baada ya kuanguka, wakati anampeleka mumewe ndani ghafla alimuona kijana mmoja ambaye alikuwa amepauka sana, kijana yule alimsalimia Ester akaitikia kwa upole,, kijana yule bila kujali kama bi Ester alikuwa anahangaika na mgonjwa, alijikuta akitoa shida yake hapohapo, " namnukuu"
"Samahani dada, hapa nilipo nilikuwa na wenzangu tunatoka field lakini tulivamiwa mstuni tulipokuwa tunafanyia field, tumenyang'anywa kila kitu, na hapa nimetembea kutoka mstuni hadi hapa kwa mguu, naomba unisaidie hela kidogo ya kunirudisha nilikotoka au chakula nile, maana sina ndugu yeyote anayenifaa zaidi ya mama tu ambaye naye ananitegemea mimi kwa kila kitu halafu yupo mbali na hapa, hata simu hana na hajui kama mwanae nimepata tatizo"
Alizungumza kijana yule mneno ambayo yalimgusa sana Bi Ester ambaye naye alikuwa amebaki na mama tu baada ya baba yake kufariki, ubaya zaidi hata mama yake alikuwa akimtegemea yeye tu licha ya kuwa na watoto wengi ambao hawakuwa na msaada wowote kwa mama yao,
***********************
"Bi Ester alimuangalia kijana yule kwa huruma kisha akamwambia asubiri, alishangaa kwanini mungu anampa majaribu namna ile na kupitia wakati mgumu kama ule, alimpeleka mumewe na kumlaza ndani huku yeye akiingia chumbani kwake na kuvuta droo akachukua pesa kiasi na kutoka nje, alipofika alimpa kijana yule ambaye hakuamini, alimuangalia mara mbilimbili bi Ester,
"Wahi sasa ukatafute usafiri maana unakoenda ni mbali sana"
Alizungumza Ester na kumfanya kijana yule kutoa machozi ya furaha kwa kutoamimin, alimuaga Ester huku akimpa maneno mazuri kwa kumuahidi mungu angetenda muujiza mkubwa sana kwa mgonjwa wake kisha akaondoka,
"Ilipita wiki moja tu kama utani Hali ya Jonathan ikatengemaa kabisa, ugonjwa uliokuwa unamsumbua ukapona kabisa na kumfanya Ester na nduguze Jonathan kujawa na Furaha,,,
_______BAADA YA MIEZI MIWILI____
"Ilipita miezi miwili, ule ugonjwa aliokuwa ameugua Jonathan ukampata Ester,Jonathan alijikaza kumhudumia ester kwa wiki moja tu ya kwanza, ndugu zake wakaanza kumwambia anaharibu mali, wapo waliomwambia kuwa Ester ndo alimloga mumewe mara ya kwanza na sasa ugonjwa umemrudia yeye, Jonathan hakukumbuka tena fadhila alizotendewa na mkewe alipokuwa mgonjwa, alichoangalia ni mali yake na hakutaka kuendelea kuiharibu kumuuguzia Ester, alichokifanya ni kumrudisha Ester kwa mama yake ambaye nae alikuwa hana uwezo na alikuwa akimtegemea sana mwanae kwenye mambo mengi.
********************
"MAma Ester hakuwa na uwezo wa kumzuia Ester kukimbia kwani tayari alikuwa ameshazeeka, Ester alikimbia na mimba yake na kuanza kuzulura barabarani kama mwehu sasa, miezi miwili mingine ilikatika huku Mama ester akimtafuta mwanae kila kona bila mafanikio, wakati huo Ester akiwa chini ya ghorofa kubwa la wahindi alikuwa akilia kwa maumivu makali ya tumbo la kujifungua wakati huo kuna gari ilipaki karibu sana na yeye, alishuka kijana mmoja akiwa na bahasha ya khaki mkononi, alipomuona Ester alijikuta akiangusha bahasha ile huku akikimbilia haraka ndani ya ghorofa lile, na baada ya muda alirudi akiwa na vijana wenzake wasiopungua watatu,walimbeba Ester na kumuingiza ndani ya gari huku kijana yule akiondoa gari kwa kasi sana,,,
"huku nyumbani kwa Jonathan baada ya kumfukuza ester alioa mwanamke mwingine ambaye alikutana naye kwenye mihangaiko ya biashara,,,laiti angejua mwanamke yule hakuwa mtu wa kawaida asingethubutu, kama kawaida ya mapenzi mapya baada ya kumuoa tu alimueleza siri zake nyingi sana,,,
"_____BAADA YA MWEZI MMOJA______
"Mwezi ulikatika wakati huo Ester ndo akili za kawaida kumrudia,alishangaa kujikuta akiwa amelala kwenye kitanda cha hospitalini,alipoangakia pembeni alimuona mama yake mzazi akiwa amebeba katoto kadogo,,
"Mamaaa nimefikaje hapa"?
aliuliza Ester ila kabla hajajibiwa kuna kijana aliingia akiwa amevaa nguo za kidokta, alimsalimia Ester na kumpa pole wakati huo Ester akiwa anashangaa,kija
na yule alianza kwa kujitambulisha
"Bila shaka umeshanisahau,Mimi ndo yule kijana ulinisaidiaga pesa kipindi fulani nilipokuja kwako nikiwa natoka field baada ya kutekwa na majambazi mstuni"
baada ya maneno yale Ester alikumbuka kila kitu na kujikuta akibubujikwa na machozi,kijana yule alijitaidi kumbembeleza Ester hadi akanyamaza,,
"Nitaishije na mtoto wangu jamani,mama yangu pia ananitegemea Mimi,mume wangu kanifukuza kisa kuugua kwangu,,,eeeh mungu weeee"
alilia Ester
"Usilie Dada, kwakuwa hauna kazi nitasubiri mwanao akue kidogo nitakufungulia mradi,pia kuhusu sehemu ya kuishi usijali,kuna nyumba nimenunua ina vyumba vingi utakuja kuishi pale na mama"
alijibu kijana yule
Ester alimungalia sana kijana yule kwa kutoamini ila alishangaa kumuona mama yake akiinuka akamsogelea mwanae akamshika mkono na kumwambia,,,
"Ni kijana mzuri sana, ndiye aliyelipia pia gharama zote za matibabu na amenihudumia wakati wote ulipokuwa mgonjwa"
hapo ndipo Ester akakumbuka alikuwa mgonjwa kweli,alisimana akamkumbatia yule kijana huku kila mmoja akitokwa na machozi
______BAADA YA MIEZI MITATU___
"Baada ya miezi mitatu tayari Ester alikuwa kwenye duka kubwa la nguo alilofunguliwa na kijana yule huku akiishi kwenye nyumba nzuri ya kijana yule na mama yake na mtoto wake,,,
"Siku moja akiwa dukani kwake, alishangaa kumuona yule kijana akipaki gari yake huku akimwambia Ester kufunga duka maana kuna tatizo imetokea,Ester alifunga haraka wakaingia ndani ya gari na kuondoka, baada ya muda walifika hospital kijana yule alimvuta mkono na kuingia kwenye moja ya chumba cha wagonjwa mahtuti, moyo ulimuenda mbio Ester baada ya kumuona mumewe akiwa amelazwa,Jonathan alipomuona mkewe alimuangalia kwa jicho regevu kwani hakuwa na nguvu tena kutokana na majeraha makubwa aliyokuwa nayo mwili mzima yakionekana ni majeraha ya moto,,
"NISAMEHE MKE WANGU, NILIKUACHA KWA KUDHANI UTAMALIZA MALI ZANGU KWA AJILI YA KUKUTIBU KUMBE NILIKUWA NAJIDANGANYA MAANA BAADA YA KUKUACHA NILIOA MWANAMKE MWINGINE NDO ALIYENIFANYIA HII NJAMA NA KUIBA MALI ZOTE KISHA AKACHOMA MOTO NYUMBA ILI KUONDOA USHAHIDI, ILA NASHUKURU WAMEMKAMATA WAKATI ANATAKA KUKIMBIA"
alizungumza Jonathan kwa shida huku akishika mkono wa mwanae, wakati anaushika tu, hapohapo akanyamaza kimya na kupoteza maisha,,,
Ester aliangua kilio kwani alikuwa bado anampenda sana mume wake,,,alimgeuk
ia kijana yule akamkuta naye akilia kwa uchungu
"pole dada nilipomuona nimemtambua kuwa ni mumeo kwani ndo nilikuta unamhudumia kipindi kile, nashangaa ulipougua ww alishindwa kukumbuka fadhira zako, hili nimejifunza hata Mimi nikioa natakiwa kumuheshimu mke wangu kwenye shida na raha,,,,
alizungumza kijana yule,,,
_______________________________
=>Pesa ni kama maua huwezi kulinganisha na uhai wa mtu
=>Usimtenge mwenzio wakati wa matatizo kwani hujui kesho yako.
=>Tenda Wema Leo,maana hujui atakaekusaidia kesho.
prepared by Emmanuel dossa
____SHARE NA WENZAKO_____