Tajiri mmoja maarufu jijini Dar, anayefahamika zaidi kwa jina moja la Salaah, amemkana muigizaji Irene Uwoya ambaye amekuwa akijinasibu kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mpenzi wake.
Kumekuwa na habari zinazozagaa mitaani kuwa Uwoya, mke wa zamani wa mwanasoka Hamad Ndikumana, ndiye anayekula maisha na mfanyabiashara huyo na kuthibitisha hivyo, muigizaji huyo ambaye yupo levo ya daraja la juu (A List Female Artist) siku chache zilizopita alionekana katika kipande cha video katika mtandao mmoja akiwa amejichora tattoo yenye jina la mvulana huyo.
“Habari kubwa mjini ni kuhusu Uwoya, inasemekana jamaa amekufa ameoza kwa shostito na mwanamke jinsi anavyojua kuweka sawa mambo kachora hadi tattoo mgongoni mwake yenye jina lake,” kilisema chanzo chetu ambacho ni miongoni mwa wasiri wa muigizaji huyo.
Risasi lilijaribu mara kadhaa kumfikia kwa njia ya simu Uwoya bila mafanikio, kwani mara zote simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu, hakujibu lolote. Salaah ambaye anadaiwa kuwa kijana mwenye fedha na anayefahamika sana miongoni mwa mastaa kutokana na ukwasi mkubwa alionao, alizungumza na Risasi Mchanganyiko akiwa nje ya nchi na kudai hajui chochote kinachozungumza juu yake na msichana huyo. “Sikiliza, mimi hayo mambo unayozungumza siyajui na wala huyo unayemtaja simjui, ndiyo kwanza nakusikia wewe, tafadhali usinihusishe na hayo mambo mimi siyajui,” alisema kwa kifupi.