Waziri wa Mambo ya Ndani na Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mwigulu Nchemba amewataka wananchi ambao wanafanya uchaguzi mdogo wa udiwani nchini wasitumie hasira kwenye upigaji kura bali wachague wagombea wa CCM ili kutimiza nguzo tatu za uongozi.
Mh. Nchemba ameyasema hayo wakati akimnadi Mgombea udiwani wa kata ya Nangwa wilaya ya Hanang ambapo amewaambia wananchi watambue kwamba serikali iliyopo madarakani inaongozwa na CCM hivyo wachague wagombea hao
Aidha Mh. Nchemba ameongeza kwamba uchaguzi mdogo ni uchaguzi rahisi sana kama watu wataamua kutafakari kwasababu ilani inayotekelezwa ni ya CCM na la pili ni huu ni uchaguzi wakujaza nafasi
"Kwasasa ilani inayofanya kazi ni ya CCM hivyo msifanye hasira katika kuchagua kwani huwezi kuwasha tochi kwa kuweka mabetri mawili ya CCM alafu la tatu liwe bunzi, Tochi haiwezi kuwaka," Mh. Nchemba
Pamoja na hayo Nchema amewataka wananchi hao waweze kumpitisha mgombea huyo mwanamke kwa kudai kwamba anafaa kuongoza na kwamba wa kina mama ni waaminifu zaidi kwani Diwani aliyepita alikuwa mwanaume lakini alihukumiwa mahakamani kwa kosa la ubadhilifu wa mali za umma