SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 17 Novemba 2017

T media news

Kamati Ya Bunge Ya Maadili Yamhoji Mhe. Kubenea Mjini Dodoma

Kamati ya  Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji  Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.

Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman  Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa  Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati  hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho   ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a)   ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.

Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika  leo (jana) baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe.

Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa  baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.