SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 17 Novemba 2017

T media news

Hatari kwa watumiaji wa mboga zinazolimwa Bonde la Mto Msimbazi, Dar

Serikali kupitia kwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji imepiga marufuku kilimo cha mbogamboga kwenye Bonde la Mto
Msimbazi jijini Dar es Salaam kutokana na maji yake kutokuwa salama na hivyo kuhatarisha afya za watumiaji wa mboga hizo.

Agizo hilo limetolewa jana Alhamsi Novemba 16, 2017 na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu bungeni mjini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum wa (CUF), Zainabu Mndolwa Amiri alitaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali kudhibiti maji yasiyo salama katika kumwagilia mboga mboga.

Wakati akijibu swali hilo, Naibu Waziri alipiga marufuku kilimo cha mboga mboga kwenye bonde hilo huku akiziagiza halmashauri za manispaa ya Jiji la Dar es Salaam kutungia sheria ndogo ndogo zikiwamo za kudhibiti matumizi ya maji hayo yenye kemikali na kinyesi kitokanacho na kadhia ya utiririshaji wa maji ya chooni jijini humo.