Inafahamika kuwa msanii wa muziki Bongo Flava, Diamond Platnumz miongoni mwa biashara anazomiliki ni Chibu Perfume na Diamond Karanga, sasa ametaja ipi inamlipa kati ya hizi mbili.
Hivi karibuni akiwa katika media tour nchini Uingereza aliulizwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ni biashara ipi inamlipa zaidi na jibu lake lake lilikuwa; ‘Off course, Diamond Karanga’. Katika hatua nyingine alizungumzia kinachomsukuma zaidi kufungua biashara mbali mbali kwa kusema kuwa anataka kutumia muziki wake katika njia ya kujinufaisha hata pale atakapoacha muziki. “Unaweza kuwa mwanamuziki lakini ukaweza kufanya vitu vingine katika misingi bora ukatengeneza ajira kwa wenzako ukatengeneza kitu ambacho hata kesho na kesho kutwa usipoweza k