SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Novemba 2017

T media news

Afande Sele " Kanumba Alivuna Alichopanda ila Lulu Unyonge wa Kisichana na Umri Vimebaki Mateso Kwake"

AFANDE SELE :

"Nikiwa kama mzazi wa mtoto wa kike ninaempenda sana na kutamani kumuona akitimiza ndoto zake muhimu kwenye maisha kama kupata elimu kwa wkt muafaka…lkn niliumia zaid baada ya matatizo aliyoyapata lulu kupitia kanumba na kwa hakika sikua miongoni mwa waliohuzunika wala kushiriki kivyovyote ule msiba wa kanumba ingawa wkt wote wa pilika za msiba ule mimi nilikua dar tena palepale sinza msiba ulipokuwepo…sikutaka kuvaa joho la unafki kama ilivyo kwa waTz wengi…kwangu hata sasa kanumba ni mtu mbaya na alifanya kitendo kibaya kabisa dhidi ya bint mdogo aliyepaswa kumsaidia kufikia malengo na sio.kumtumia kwa sababu ya umaarufu wake…leo kanumba amepumzika au anapambana na Mola wake kwa kutofuata yale maandiko yasemayo kuwa’TAMAA Ikichukua Mimba Huzaa Dhambi na Dhambi Ikishakukomaa Huzaa MAUTI…Kanumba amevuna alichopanda lkn Lulu unyonge wa kiumri na udhaifu wa kisichana vimebakia kuwa mateso ktk maisha yake…MUNGU ni mwema atamuafu Lulu amalize kifungo chake salama kama alivyompa kanumba haki ya matendo yake mabaya kwa kumlaza mapema…Mwisho wa siku wote wawili wabarikiwe kwa kutufundisha tuliobakia ili tuchague njia sahihi za kupita….DUNIA..GUNIA"