Mahakama Kuu ya Tanzania, leo Novemba 13 imemhukumu kwenda jela kwa miaka miwili mwigizaji wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba.
Elizabeth ambaye pia ni maarufu kwa jina la Lulu amekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba, tukio lililotokea Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam.
Baada ya mahakama kutoa hukumu hiyo watu mbalimbali wameandika katika mitandao ya kijamii wakieleza maoni na hisia zao kuhusu hukumu hiyo, huku baadhi wakisikitika lakini wengine wakisema kwamba sheria ndio njia pekee ya kutenda haki, hivyo hukumu hiyo imeonyesha haki imetendeka.
Bali na watu hao, waigizaji na watu wengine nao wameandika yao kuhusu hukumu hiyo, hapa chini ni baadhi ya wasanii na viongozi walioandika kuhusu kufungwa kwa Lulu.
“Mwenyezi Mungu ameamua kukupa mtihani huu wewe kwasababu anaamini wewe ni Shujaa na Imara…..pia anaamini wewe ndio msichana pekee unaeweza kuuhimili mtihani huu…. hivyo Usisononeke, Make him Proud!!!”- Diamond Platnumz
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameandika, “There is a room in every situation. Stay strong, Dady is coming!,” akimaanisha kuna njia katika kila jambo. Simama imara, Baba anakuja.
Mwigizaji Wema Sepetu, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika, “Dah… Speechless…
Pole my baby… This too shall pass…
.”
Dk Cheni ambaye amekuwa karibu sana na Lulu katika safari yake ya uigizaji aliandika, “Linapokukuta jambo wapo wakaokuonea huruma na wapo watakaokuwa na furaha ila niwakumbushe jambo akuna ajuwaye kesho yake kubwa kila mapito mwambie Mungu Asante.”