SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 17 Oktoba 2017

T media news

Marekani Yataka Utulivu Baada ya Iraq Kuteka Mji wa Kirkuk

Marekani imeombakuwepo utulivu baada ya wanajeshi wa serikali ya Iraq kuteka mji wa Kaskazini mwa Iraq wa Kirkuk na vituo muhimu kutoka kwa wakurdi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Heather Nauert amezitaka penda zote kuzuia makabiliano zaidi.
Wanajeshi wa Iraq walielekea Kirkuk wiki tatu zilizopita, baada ya eneo la Kurdistan kuandaa kura ya maoni ya uhuru iliyokumbwa na utata.
Wanajeshi wa Iraq waingia Kirkuk, Wakurdi watoroka
Lengo lao ni kuteka sehemu zilizo chini ya udhibiti wa wakurdi tangu Islamic State wadhibiti eneo hilo.
Wenyeji wa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa wakurdi ukiwemo mji wa Kirkuk, kwa wingi waliunga mkono kujitenga kutoka Iraq wakati wa kura ya tarehe 25 mwezi Septemba.

Licha ya mji wa Kirkuk kuwa nje ya eneo la Kursistan, wapigaji kura wa Kurdistan walio mjini humo waliruhusiwa kushiriki kura.
Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi aliitupilia mbali kura hiyo na kuitaja kuwa iliyo kinyume na katiba.
Wakurdi wa Iraq wanasema wako tayari kujitenga na kuwa na taifa lao
Huku hayo yakijiri, wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali wamechukua udhibiti wa mji wa Sinjaar Kaskazini magharibi mwa mkoa wa Nineveh.
Hatua hiyo katika mji unaodaiwa na wakurdi na pia mamlaka za Iraq, ilifanyika bila ya kuwepo mapigano baada ya wanajeshi wa wakurdi wa Peshmerga kuondoka eneo hilo.

Katika taarifa Bi Nauert alisema kuwa Marekani ina wasi wasi kutokana na ripoti za kuendelea mapigano katika mji wa Kirkuk.
Bi Nauert alisema kuwa Marekani ilikuwa ikishirikiana na maafisa kutoka pande zote, kushiriki mazungumzo ikionya kuwa bado kuna kazi kubwa ya kulishinda kundi la Islamic State nchini Iraq.
Mapema Rais Donald Trump alikuwa amesema kuwa maafisa wa Marekani hawapendelei upande wowote.