Idadi kubwa ya waandishi chipukizi nchini Tanzania, wanakabiliwa na changamoto moja kubwa. Nayo si nyingine isipokuwa ni kushindwa kufikia ndoto ya kuchapisha walau kitabu kimoja kwa sababu ya kutokumudu gharama za uchapishaji wa vitabu.
Kuchapisha kitabu chenye kiwango ( standard ) kinacho hitajika sokoni, ambacho kinaweza kukubaliwa na wauzaji na wasambazaji wakubwa nchini, mwandishi anatakiwa kwa kadirio la chini kabisa, awe na walau kiasi cha shilingi LAKI NANE hadi MILIONI MOJA NA NUSU kutegemea na ukubwa wa kitabu.
Kiasi hiki kinaonekana kuwa kikubwa mno kwa mwandishi chipukizi ambae ndio kwanza anataka kutumia kipaji chake cha uandishi kujipatia fedha kwa ajili ya kuendesha maisha yake ya kila siku na kupata maendeleo kwa ujumla.
Mwisho wa siku waandishi hawa huamua kukata tamaa ya kutimiza ndoto yao hiyo adhimu na matokeo yake mawazo waliyo taka kuyaandikia kitabu hufa ama kupotea.
SULUHISHO LA CHANGAMOTO HII
Katika kukabiliana na changamoto hii, kampuni ya masoko ya MWALU MARKETING & GENERAL ENTERPRISES imenzisha program maalumu ya kuwasaidia waandishi chipukizi kuchapisha mawazo yao kwenye kitabu kwa gharama nafuu kabisa ambazo wanaweza kuzimudu.
Badala ya mwandishi mmoja, kutoa gharama ya SHILINGI LAKI NANE kwa ajili ya kuchapisha kitabu chake, Mwalu Marketing inawakusanya waandishi chipukizi kuanzia kumi wenye mawazo yanayo fanana na kuchapisha kitabu kimoja ambapo kila mwandishi atatakiwa kutoa kiasi cha SHILINGI ELFU THEMANINI TU (Tshs . 80,000/=).
Program hii imelenga kuwasaidia maelfu ya waandishi chipukizi wa vitabu nchini Tanzania, ambao wanatamani kuyaweka mawazo yao kwenye vitabu lakini wanashindwa kwa sababu tu hawana uwezo wa kumudu gharama kubwa za uchapishaji.
TUNAPOKEA MAOMBI YA WAANDISHI CHIPUKIZI WANAO TAKA KUSHIRIKI KATIKA PROGRAMU.
Kama wewe ni mwandishi chipukizi ambae unatamani kuchapisha kitabu ama kuweka wazo lako kwenye kitabu lakini hauna pa kuanzia kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama kubwa za uchapishaji, basi hii ni HABARI NJEMA SANA KWAKO.
Kwani kupitia program hii, utaweza kuweka wazo lako kwenye kitabu kwa gharama ya SHILINGI ELFU THEMANINI TU (Tshs.80,000/=)
SIFA ZA KITABU
Ili kitabu chako kiweze kukwekwa kwenye program hii ni lazima kiwe na sifa zifuatazo :
1. Kiwe na maudhui mazuri na yenye kuvutia yasiyo kinyume na maadili ya mtanzania.
2. Kiwe na maudhui yanayo zingatia na kufuata taratibu na sheria za nchi.
3. Kisiwe na maudhui ya kisiasa au yenye mwelekeo wa kisiasa.
MAUDHUI YATAKAYO PEWA KIPAUMBELE
Maudhui yatakayo pewa kipaumbele katika program hii ni pamoja :
1. Riwaya mbalimbali za kusisimua
2. Simulizi kuhusu historia ya ukweli ya maisha ( IWE SIMULIZI YENYE KUSISIMUA )
3. Mafundisho mbalimbali ya ujasiriamali kama vile :
i. Utengenezaji na utayarishaji wa bidhaa mbalimbali
ii. Ufugaji wa mifugo mbalimbali kama vile kuku wa kienyeji, kuku wa nyama na kuku wa mayai, mbuzi wa nyama & maziwa, ng’ombe wa nyama na maziwa, nakadhalika.
iii. Kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara
iv. Fursa za biashara mbalimbali na ujasiriamali
v. Uanzishaji na uendeshaji wa biashara mbalimbali
vi. Uanzishaji na uendeshaji wa makampuni mbalimbali
vii.Uanzishaji na uendeshaji wa Taasisi na mashirika mbalimbali
viii. Uanzishaji na uendeshaji wa viwanda vidogo vidogo vya aina mbalimbali kama vile viwanda vya usindikajiwa bidhaa mbalimbali nakadhalika.
ix. Usagaji na upakiaji wa unga wa mahindi, muhogo nakadhalika.
x. Uanzishaji na uendeshaji wa biashara ndogo za aina mbalimbali .
xi. Mafunzo ya ufundi stadi.
4. Uandishi wa vitabu vya kitaaluma vya masomo mbalimbali kuanzia ngazi ya chekechea.
5. Uandishi kuhusu umuhimu na faida za kusoma kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti nakuendelea zinazo tolewa na vyuo mbalimbali
6.Uandishi kuhusu historia na shughuli za Taasisi mbalimbali zisizo kuwa za kiserikali (NGOS)
7.Uandishi kuhusu historia na shughuli za kampuni mbalimbali
8. Uandishi kuhusu utelekezaji wa miradi ya mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali ( NGOS )
9. Vitabu kuhusu mafundisho ya kidini
10. Vitabu kuhusu mafundisho ya afya
11. Vitabu kuhusu masuala ya jadi na utamaduni
12.Uandishi wa mashairi ya muziki wa bongo fleva ( Katika maudhui mbalimbali kuanzia R& B hadi HipHop ) :HII INAWAHUSU WATUNZI WA MASHAIRI YA NYIMBO ZA BONGO FLEVA AMBAO WANATAKA KUONYESHA VIPAJI VYAO VYA UTUNZI KUPITIA KITABU )
13. NAKADHALIKA.
JINSI YA KUFANYA
Fika katika ofisi zetu zilizopo MBEZI BEACH jijini DAR ES SALAAM ukiwa na manuscript ( muswaada) wa kitabu chako katika soft copy .
NA KWA MAELEZO NA UFAFANUZI ZAIDI, WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA : 0787 01 69 29
Kwa waandishi chipukizi waliopo nje ya mkoa wa Dar Es Salaam, ambao wanataka kushiriki katika program hii wasiliana nasi kwa simu yetu 0787 01 69 29 tuwape utaratibu.
WAHI NAFASI YAKO MAPEMA,KABLA OFA HII HAIJA FIKA TAMATI.