SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Septemba 2017

T media news

Wazee wa Manispaa ya Ubungo Wapata Neema

Wazee zaidi ya 7,000 wa Manispaa ya Ubungo, wamekabidhiwa vitambulisho vya msamaha wa wa matibabu bure kwa wazee ili kuwasaidia wasiojiweza kupata huduma hiyo.

Mpango huo umezinduliwa leo Jumatatu na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambapo alikabidhi kadi hizo kwa wazee zaidi ya 100 kwa niaba ya wenzao katika viwanja vya Tip -Sinza.

Mwalimu ameeleza kufurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Manispaa ya Ubungo kwa kutimiza ahadi ya Rais John Magufuli ya  kuweka  utaratibu huo wa matibabu bure.

"Nimefurahishwa na hatua hii. Leo natangaza ramsi mmeingia katika rekodi zangu za kuwa manispaa inayowajali wazee. Mimi mwenyewe niwahi kukaa Ubungo wakati nasoma chuo kikuu mlimani nawashukuru sana kwa jambo hili,"amesema Mwalimu.

Amesema wazee wana changamoto mbalimbali ikiwamo kipato kidogo jambo linalosababisha miongoni kushindwa kupata matibabu kwa ufanisi hivyo hatua hiyo itasaidia kupata huduma hizo.

Aliongeza kuwa ni hatua hiyo ni njia ya kuwaelekea katika bima za afya kwa wazee kama mkakati wa Serikali wa kuwasaidia wazee hao.

Mwalimu alitumia nafasi kuwaihidi viongozi wa manispaa ya hiyo atawajengea wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji katika mojawapo ya vituo vya afya vya Ubungo.

Meya wa Ubungo,  Boniface Jacob amesema  manispaa hiyo imejipanga ipasavyo katika kuhakikisha wazee wanapata huduma hiyo ya bure.

"Wengine walizani ni utani, nawaambia sisi hatuna mzaha ndiyo maana leo tumemwita waziri kuja kuzindua. Kauli mbiu yetu ni 'mzee kufa kwa kukosa matibabu sasa basi',"amesema Jacob.w