SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 12 Septemba 2017

T media news

Rais Mstaafu wa Senegal ajiuzulu ubunge

Rais Mstaafu wa Senegal, Abdoulaye Wade amejiuzulu nafasi yake  ya ubunge aliyoshinda takribani mwezi mmoja uliopita siku chache kabla ya mkutano wa Bunge kuanza Alhamisi Septemba 14 mwaka huu.

Wade mwenye umri wa miaka 91 alishinda kiti cha ubunge Julai 30 mwaka huu kupitia chama cha upinzani cha Democratic Party kilichokuwa miongoni mwa vyama vilivyounda muungano katika uchaguzi wa nchi hiyo.

Rais hiyo alitangaza kujiuzulu jana Septemba 11 kupitia barua yake ambayo ilichapishwa katika vyombo vya habari nchini humo ambapo alisema aligombea ili kukisaidia chama hicho pamoja na muungano huo wa upinzani.

Chama cha Wade kilishinda viti 19 huku chama tawala kikishinda viti 125 kati ya viti 195 katika bunge la nchi hiyo.

Wade alirejea chini humo kutoka Ufaransa siku 3 kabla ya uchaguzi kwa ajili ya kuja kufanya kampeni.

Abdoulaye Wade alikuwa Rais wa Senegal kwa kipindi cha miaka 12 tangu mwaka 2000 hadi 2012.

Baada ya kutangazwa kuwa mshindi, ilielezwa kuwa Wade angekuwa mbunge mwenye umri mkubwa zaidi dunia kama angeamua kutumikia wadhifa huo.