WASWAHILI wanasema mwenzako akinyolewa, wewe tia maji nywele zako, sina hakika kama Uchebe, ambaye ni mpenzi mpya wa Diva kutoka kiwanda cha Bongo fleva na muvi, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ alijipanga kukutana na mbilingembilinge zilizowahi kuwakuta wapenzi wa mwanadada huyo, akiwemo mwanamuziki Nuh Mziwanda.
Mara zote Uchebe alikuwa akiposti picha na kuandika ujumbe mzito wa kumsifia mpenzi wake huyo na kuwataka vizabizabina wakae kando, kwani wapo kwenye dimbwi zito la mahaba. Mashabiki wanadai kwamba kwa sasa hali si shwari baina ya wapenzi hao, na hii ni kutokana na posti yake ya hivi karibuni, kuwa haina uwiano na zile za mwanzo.
Kupitia ngoma yake ya ‘Jike Shupa’, Nuh Mziwanda alielezea tabia za Shishi, kwamba ni mwanamke mbabe, anayependa kusikilizwa, sifa ambazo zina fanana kidogo na posti ya Uchebe.