SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 7 Septemba 2017

T media news

MTAZAMO: Shaffih Dauda, Edgar Kibwana, baada ya Buswita kufutiwa adhabu ya kufungiwa

Wachambuzi wa michezo wa kituo cha Clouds Media Group mkongwe Shaffih Dauda pamoja na Edgar Kibwana kila mmoja ametoa mtazamo wake baada ya kamati ya sheria, katiba na hadhi za wachezaji kumfungulia kifungo mchezaji Pius Buswita ambaye awali alifunguwa kwa kusaini mikataba ya kuzichezea timu mbili tofauti (Simba na Yanga) ndani ya msimu mmoja.

Buswita ameruhusiwa kuitumikia Yanga kwa sharti la kuilipa Simba gharama walizotumia kumsainisha mkataba ikiwa ni baada ya vilabu hivyo kukubaliana kumalizana, kamati ikabariki maamuzi yao kwa kutoa sharti kwa Buswita kuilipa klabu ya Simba kabla ya kuanza kucheza akiwa na jezi za Yanga.

Kibwana amesema kwamba, ukiangalia rekodi kuna wachezaji ambao walifungiwa kwa kusaini mikataba ya kuzityumikia timu mbili tofauti na walitumikia adhabu zao akiwepo mchezaji wa zamani wa Tanzania Prisons Mohamed Mkopi ambaye alisaini Mbeya City wakati bado ana mkataba na Prisons.

“Klabu kukubaliana haiondoi dhana ya kurekebisha makosa kama haya ili iwe onyo kwa wachezaji wengine ambao watafanya vitendo kama hivi,” Edgar Kibwana kuhusu kuondolewa adhabu ya kufungiwa Pius Buswita”-Edgar Kibwana.

Kwa upande wa Shaffih Dauda yeye amesema tatizo la mchezaji kusaini mikataba miwili kucheza timu mbili tofauti au kusaini mkataba na timu nyingine ikiwa bado ana mkataba na timu yake ya awali anaepaswa kulaumiwa ni mchezaji husika.

“Matatizo haya mimi naendelea kumbebesha ,mchezaji alikuwa anajua kwamba ameshasaini mkataba na klabu mmoja hakukuwa na sababu ya kusaini kwingine na haiwezekani kwamba mikataba aliisaini kwa wakati mmoja.”

“Hakukuwa na haja ya kufanya uhuni alioufanya, na hiyo hela inayotakiwa kulipwa ingebidi alipe yeye mwenyewe hata kama klabu italipa ili imtumie basi akatwe kwenye mshahara wake kufidia ili wakati mwingine asifanye uhuni.”

Katika maoni yake Dauda ametoa angalizo kwa TFF kutofanya double standard, hatua zinazochukuliwa kwa wachezaji wa timu ndogo ziwe sawa na kwa wale wa Simba na Yanga lakini ikitokea wachezaji wa wengine wanapendelewa kwa sababu tu wanacheza Simba au Yanga ni hatari kwa maendeleo ya soka la Tanzania.

“Kusifanyike double standard kwa sababu mchezaji anavihusu vilabu vya Simba na Yanga anatafutiwa namna ya kutoka. Wawaangalie na wachezaji wa vilabu vingine vidogo,” Shaffih Dauda kuhusu Buswita kuondolewa adhabu ya kufungiwa kwa kusaini mikataba timu mbili”-Shaffih Dauda.