SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 2 Septemba 2017

T media news

Mchezaji wa Azam amepelekwa Afrika Kusini kufanyiwa upasuaji

WINGA wa kushoto wa Azam FC, Joseph Kimwaga, amepelekwa Afrika Kusini kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kushoto. Kimwaga ameondoka Ijumaa September 1, 2017 akiwa pamoaja na daktari wa timu Mwanandi Mwankema.

Kimwaga aliteguka goti Alhamisi iliyopita kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu cha TTC cha mkoani Mtwara, wakati Azam FC ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ndanda ulioisha kwa Azam kushinda bao 1-0 wikiendi iliyopita.

shaffihdauda.co.tz inaungana na Azam FC pamoja na wanafamilia ya mpira wa miguu Tanzania kumuombea Kimwaga matibabu yake yaende vizuri na aweze kurejea uwanjani haraka kuitumikia timu yake.

Chanzo: azamfc.co.tz & azamfcofficial instagram account.