Timu ya taifa ya Hispania wakiwa nyumbanj wakiwa ugenini waliichakaza Liechteinstein mabao 8 kwa nunge huku Alvaro Morata akifunga 2, Iago Aspas 2, Sergio Ramos 1, Isco 1, David Silva 1 na Maximillan Gopell akijifunga.
Italia waliichakaza Israel bao 1 kwa nunge bao likifungwa na Ciro Imobille, Austria walisuluhu bao moja kwa moja na Georgia huku Turkey wakiifunga Croatia bao moja kwa nunge.
Huku barani Africa Dr Congo walisuluhu na Tunisia huku magoli ya Congo yakiwekwa kambani na Jose Mpoku na Mubele Ndombe, huku ya Tunisia yakifungwa na Anice Badri huku Wilfred Moke akijifunga.
Gabon pamoja na kuwa pungufu waliishangaza Ivory Coast kwa kuipiga 2 kwa 1 nyumbani kwao huku mabao ya Gabon yakifungwa na Axel Meye na Mario Lemina,Ivory Coast bao lao likifungwa na Michael Serri.
Majirani zetu Uganda walifungwa bao 1 kwa nunge na timu ya taifa ya Misri kwa bao la Mohamed Salah huku Mali na Morocco wakimaliza mchezo wao kwa suluhu ya bila kufungana.
South Africa walifungwa na Cape Verde bao 2 kwa 1, mabao ya Cape Verde yalifungwa na Garry Rodriguez aliyefunga mara mbili huku South Africa wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Andile Jali.