SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 3 Septemba 2017

T media news

Majeruhi Asimulia Alivyonusurika Kuuawa na Chui Mwanza

Miongoni mwa Taarifa za kusikitisha kutoka Mwanza ni pamoja na tukio la usiku wa kuamkia September 1, 2017 ambapo watu watano; wawili wakiwa ni Askari wa Wanyamapori, wiwili ni Askari Polisi na raia mmoja kujeruhiwa na Chui katika kijiji cha Kabangaja, Igombe Ilemela.

Mmoja wa majeruhi Otienel Mwihomeke ameelezea tukio hilo akisema wakiwa kazini usiku huo walipewa taarifa kuwa kuna mwananchi mchunga ng’ombe amevamiwa na chui hivyo kuamua kwenda kutoa msaada ambapo baada ya kufika Chui alikimbilia kichakani kujificha na Afisa mmoja wa wanyamapori aliposogelea eneo hilo alivamiwa na chui huyo kisha akarudi tena kichakani.

”Baada ya muda mfupi Chui alirudi na kumvamia Askari mwingine aliyesimama karibu yangu na nilipojaribu kusaidia kumtoa, Chui alinivamia na mimi na kuning’ata mkono na baadaye alikimbia kurudi kichakani.” – Otienel Mwihomeke.