SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 12 Septemba 2017

T media news

Kamera ya Kupiga Picha Ndani ya Mwili wa Binadamu yatengenezwa

Wanasayansi wamebuni kamera yenye uwezo ya kupiga picha viungo vya ndani ya mwili wa binadamu, BBC imeripoti.

Kifaa hicho kimeundwa kuwasaidia madaktari kusaka vifaa vya madaktari, vinavyofahamika kama endoscopes, ambavyo huenda vinaweza kusalia ndani ya viungo vya binadamu wakati wa upasuaji.

Hadi sasa, matabibu wamekuwa wakitegemea uchunguzi unaogharimu vifaa vya bei ghali, kama vile picha za X-ray, ili kufuatilia mafanikio yao.

Kamera hiyo mpya, itafanya kazi ya kubaini mwanzo wa mwangaza ndani ya mwili wa binadamu, kama vile sehemu ya ncha ya mwisho ya kifaa cha upasuaji cha tube ya endoscope.

Profesa Kev Dhaliwal, wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, anasema: “Ina uwezo mkubwa wa kutumika katika hali tofauti tofauti, kama vile inavyoelezwa ikiwa kazini. “Uwezo wa kuona kiliko kifaa kilichosahaulika ndani ya mwili wa binadamu hasa katika sekta mbalimbali ya kitengo cha kiafya, huku tukisonga mbele kupunguza hali na mbinu ya kila aina ya kutibu maradhi mbalimbali.”

Kamera ya kupiga ndani ya mwili wa binadamu
Majaribio ya awali, inaonyesha kifaa cha prototype, kinaweza kubaini na kufuatilia mwangaza kupitia eneo la mshipa wa sentimita 20, katika hali tu ya kawaida.

By Tekno Kona