SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 12 Septemba 2017

T media news

Dawa Mbadala 9 Zinazotibu Ugonjwa wa U.T.I

U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu.

Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.

Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra.

Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.

Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Kinachosababisha U.T.I:
Kisukari
Maumivu ya mishipa
Ajari katika uti wa mgongo
Ushoga (kwa wanaume)
Usafi duni
Upungufu wa maji mwilini
Kushikilia mkojo muda mrefu
Kurithi
Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.

Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I

Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
Kukojoa mara kwa mara
Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
Mikojo kukutoka pasipo kutaka
Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
Kukojoa damu
Harufu nzito au mbaya ya mkojo
Homa
Kusikia baridi
Kutokujisikia vizuri
Kujisikia uchovu

Dawa mbadala 9 zinazotibu U.T.I

1. Baking Soda

U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kupelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi.

Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I.

Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka.

Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.

2. Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries):

Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I.

Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu.

3. Nanasi

Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain’

Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I.

Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.

4. Maji

  Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji.

Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano.

Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa.

Kujifunza zaidi kuhusu tiba kwa kutumia maji bonyeza hapa.

5. Vitamini C

Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo.

Vitamini C hukifanya kibofu cha mkojo kubaki na afya kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo. Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye unga wa majani ya mlonge.

Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na U.T.I.

Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bakteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo.

Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I.

Namna ya kukitumia; Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe na uchukuwe punje 6, menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa nyingine yoyote na maji vikombe 2 (nusu lita) kila unapoenda kulala kwa siku 7 hivi au zaidi.

7. Limau/ndimu:

Weka vijiko vikubwa vitatu vya juisi ya limau au ndimu ndani ya glasi moja ya maji (robo lita) na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara tatu.

Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.

8. Unga wa majani ya Mlonge

Tumia kijiko kidogo kimoja cha chai ndani ya uji,  au ndani ya juisi  ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani, au katika maji ya uvuguvugu kutwa mara 1. Tumia kwa wiki 3 mpaka mwezi mmoja.

9. Mshubiri (Aloe-Vera):

Chukua jeli ya mshubiri (aloe-vera) vijiko vikubwa viwili, changanya na maji ya kawaida ili kupata kikombe kimoja (ml 250) au robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 1 kwa siku 3 hadi wiki 2 au hadi utakapopona.

Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.

Vitu vya kufanya kujikinga usipatwe na U.T.I

Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
Penda kuwa msafi.
Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma (hasa kwa wanawake) na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
Jisafishe vizuri mara baada ya tendo la ndoa.
Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda
Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
Epuka kaffeina.
Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.
Dawa mbadala hizi 9 zinaweza kukusaidia kujikinga usipatwe na U.T.I au kujitibu ingawa bado inashauriwa kwenda kumuona daktari iwapo maumivu au dalili zinadumu kwa muda mrefu.