SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 5 Septemba 2017

T media news

Buffon amtaja mshambuliaji hatari zaidi kuwahi kukutana naye, sio Messi wala Cr7

Golikipa mkongwe wa timu ya taifa ya Italia ambaye pia anaichezea Juventus Gianluigi Buffon anasifika sana kwa kuzuia mashambulizi wa wapinzani na kuokoa michomo inayoelekezwa golini mwake.

Washambuliaji wengi wamekuwa wakupata tabu sana wanapocheza dhidi ya Buffon lakini golikipa huyo naye amekiri kwamba kuna mshambuliaji mmoja ambaye alikuwa akimpa tabu sana akicheza dhidi yake.

Buffon anadai hajawahi kukutana na mshambuliaji hatari kama ilivyo kwa Ronaldo De Lima na ilikuwa ikimpa wakati mgumu sana kukabiliana naye kwani mshambuliaji huyo alikuwa ni mwiba haswa.

“Mshambuliaji aliyekuwa akinisumbua sana na kunipa wakati mgumu ni Ronaldo wa Brazil, alikuwa ana kasi sana na alikuwa ana nguvu, alikuwa kama ametengenezwa maabara” alisema Buffon.

De Lima alifunga mabao 247 katika michezo 343 aliyocheza katika ngazi za vilabu huku Gianluigi Buffon bado akihangaika na soka na leo usiku anatarajia kuidakia Italia itakapocheza dhidi ya Australia katika mchezo wa kufudhu kombe la dunia.