SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Septemba 2017

T media news

Breaking: Hii ndiyo tarehe ya uchaguzi wa marudio nchini Kenya

Tume ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC) imetangaza kuwa uchaguzi wa marudio nchini humo utafanyika Oktoba 17, 2017 baada uchaguzi wa awali ambao ulifanyika Agosti 8 mwaka huu kufutwa.

Uamuzi wa kurudiwa kwa uchaguzi nchini Kenya umefuatia maamuzi ya Mahakama ya Juu  kutangaza kwamba uchaguzi wa urais wa awali ulikuwa ni batili kutokana na kutofuata kanuni, sheria na taratibu za nchi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na tume hiyo, inaeleza kuwa kufuatia kikao kulichofanyika leo, hiyo ndio itakuwa tarehe ya uchaguzi wa marudio na kwamba wagombea watakaokuwa katika karatasi ya kupigia kura watakuwa ni wawili tu ambao ni Rais Uhuru Kenyatta ambaye mgombea mwenza ni William Ruto na Raila Odinga ambaye mgombea mwenza ni Stephen Musyoka.

Baadhi ya wagombea ambao walikuwa katika uchaguzi wa awali, wamepinga vika kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho na kusema kwamba watakwenda mahakamani kwa sababu kitendo hicho ni ubatili mtupu.

Kenya iliweka historia ya kuwa taifa la kwanza barani Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais baada ya upinzani kwenda mahakamani kulalamikia mapungufu katika zoezi zima la uchaguzi.

Kwa upande wake Kenyatta ambaye alitangazwa mshindi kwa 54% alisema kwamba hakubaliani na maamuzi ya mahakama na kwamba watu sita hawawezi wakakaa na kupinga kilichofanywa na mamilioni ya Wakenya.

Kwake Odinga alisema hiyo ilikuwa ni historia kwa Kenya, Afrika na hata dunia huku akiahidi kuwa katika uchaguzi wa marudio atashinda. Hata hivyo Odinga katika moja ya mazungumzo yake alisema kwamba hatoshiriki uchaguzi huo kama baadhi ya maofisa wa tume ya uchaguzi hawatoondolewa akidai walikuwa sababu ya kuvugika kwa uchaguzi wa awali.