SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 16 Septemba 2017

T media news

Bongo Movie Wazindua Huduma Mpya ya Kununua Filamu Kupitia Simu

Wadau wa Filamu Tanzania BARAZANI Entertainment wamezindua huduma mpya za kimtandao ambayo itamuwezesha mteja kununua filamu kupitia simu yake ya mkononi.

Mkurugenzi Mtendaji wa BARAZANI Entertainment John Kallage ameeleza kuwa kupitia huduma hii watu wataweza kununua filamu kama wanavyoweza kununua luku, ving’amuzi na huduma nyingine kama hizo na ndani ya masaa mawili baada ya kufanya malipo watakua wamekwisha kupata filamu hiyo.

Mtandao huu pia utamjulisha wa kutuma ujumbe mfupi mmiliki pamoja na wahusika waliocheza filamu hiyo kuhusu nani amenunua filamu hiyo na eneo alipo na hii itawasaidia kufatilia mapato halisi yanayopatikana kwenye filamu zao na kuepuka kudhulumiana.