KUTOKA IKULU YA MAREKANI
Washington DC
Mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya White House Anthony Scaramucci amefutwa kazi chini ya siku 10 baada ya kuteuliwa kuhudumu katika wadhifa huo.
Scaramucci, ambaye amehudumu kwa kipindi kirefu katika Wall Street, alikuwa amekosolewa sana baada ya kumpigia simu mwanahabari mmoja kuwasema wahudumu wenzake katika ikulu.
Mkuu wa utumishi wa umma wa Bw Trump Reince Priebus na msemaji wake Sean Spicer wote walijiuzulu kutokana na uteuzi wa Scaramucci.
Uamuzi wa kumfuta kazi umefanywa na mkuu mpya wa utumishi wa umma wa Trump, John Kelly, ambaye aliapishwa mapema jana Jumatatu.
Taarifa fupi ya sentensi tatu kutoka White House imesema: "Anthony Scaramucci atauacha wadhifa wake kama Mkurugenzi wa Mawasiliano wa White House.