Mshambuliaji wa timunya taifa ta Brazil na klabu ya Barcelona Neymar Dod Santos ameonekana jijini Dubai ambako inadaiwa ameenda kwa ajili ya kukamilisha usajili wake kwenda PSG.
Akiwa Dubai inadaiwa Neymar atapanda tena ndege kuelekea jiji la Doha nchini Qatar ambako ndiko wamiliki wa PSG walipo tayari kwa kusaini mkataba wa kuitumikia PSG.
Mmiliki wa PSG Nasser Al Khelaifi anaonekana anamhitaji sana Neymar sio tu kwa ajili ya soka lakini anamuhitaji kama “brand” kuitangaza Qatar katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.
Uhamisho wa Neymar kwenda PSG utaigharimu PSG kiasi cha £196 na zaidi huku Neymar akijiandaa kupokea £500,000 kwa wiki na kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi barani Ulaya.
Neymar anaonekana kuchoshwa na Barcelona haswa kutokana na uwepo wa Messi ambaye anaonekana kama anaziba nafasi ya Neymar kuwa mchezaji mkubwa zaidi na sasa naamini PSG anaenda kung’ara.