Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amenukuliwa akizima mjadala wa kuhusu goli la kusawazisha la mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara 'Yanga' dhidi ya Lipuli FC kwa kudai kuwa timu hiyo haikubebwa na goli lililofungwa ni hala
Bwire amesema anaamini bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe Donald Ngoma lilikua halali, kwani mpira ulivuka mstari wa goli na ndio maana mwamuzi aliamuru mpira upelekwe kati na sivyo kama watu wengine wanavyofikiria.
“Mimi nimeona mpira ulivuka mstari kabisa, hakuna utata wowote katika bao lile, nashangaa kuona watu wakisema Young Africans walibebwa! “Ukifuatilia vizuri ule mpira uliopigwa kwa kichwa na Ngoma, utaona dhahiri mpira ulivuka mstari, wakati mwingine wabongo wanapenda sana malumbao, na hii inatokana na ushabiki uliokithiri miongoni mwetu bila kuangalia jambo kwa umakini”, alinukuliwa
Ameongeza kuwa “Siwatetei Young Africans, ninasema kile nilichokiona katika mchezo wa jana ambao hata hivyo ulikua mzuri na wa kuvutia, kutokana na kikosi cha Lipuli kuonyesha soka safi ambalo liliwafanya wapinzani wao wasifurukute kabisa”