SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Agosti 2017

T media news

Idris Sultani Ampigia Saluti Joti Awataka Mashabiki Wake Wasimlinganishe Naye

Mchekeshaji na Muigizaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultan ameweka wazi kwa kuwambia mashabiki wake waache kumfananisha na mchekeshaji mkongwe, Joti kwani kufanya hivyo ni kumvunjia heshima yake.

Idris Sultan amesema amekuwa akisikia minong’ono kutoka kwa wadau wa burudani wakimfananisha na Joti kitu ambacho yeye binafsi hakipendi kwani hadi kufikia hapa alipo ni kutokana na kujifunza kutoka kwa wakongwe wa tasnia ya uchekeshaji akiwemo Joti.

“Kuna kauli flani inasema Joti mkali kuliko Idris mara wengine wakisema Idris new generation comedy yuko vyema sana na blah blah nyingi ila tunasahau mkondo wa heshima na kuelewa kuwa Joti ni babu yangu kabisa yani kama tutasherehekea industry ya comedy naomba Joti asifananishwe na vitu vya kijinga kama mimi. Legends wapo level yao wenyewe”,ameandika Idris Sultan kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akikiri wazi kuwa kipaji cha Joti atabaki kuwa Joti na ataendelea kummheshimu siku zote.

“Narudi chini kidogo na kuinamisha kichwa naiacha heshima itutangulie na naomba nikushukuru sana Joti kwa kutuwekea mazingira uliyotuwekea wote tunaojaribu na wote wanaonifata”,ameandika Idris Sultan.

Idris Sultan ameendelea kuvuna idadai ya mashabiki nchini Tanzania kupitia kipaji chake cha uigizaji ingawaje kumekuwa na changamoto ya soko la aina ya uchekeshaji anaoufanya ‘Uchekeshaji Wima’ (Stand up Comedian).