Muendelezo wa wabunge wa upinzani kutiwa nguvuni kwa tuhuma mbalimbali umezidi kushika kasi baada ya leo Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe, Pascal Haonga, kukamatwa na Polisi leo mchana akiwa katika mji mdogo wa Mlowo-Mbozi.
Mbunge huyo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi na kufanya mkusanyiko usio halali.
Licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange, kuthibitisha kumshikilia Haonga lakini hakutaka kueleza suala hilo kwa kina kwa madai kuwa hayupo ofisini.
Meshack Mgaya ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Songwe amesema kuwa chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu kukamatwa kwa kada huyo na kwamba baada ya kujiridhisha watato tamko.