Msanii wa bongo fleva, Nuh Mziwanda amefunguka kwa kudai chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake ni kutokuwa na pesa za kutosha za kuweza kuwahudumia familia ya mke wake kama alizokuwa nazo mwanaume aliyemuoa Nawal hivi karibuni.
Nuh Mziwanda amebainisha hayo, baada ya kila kitu mtu kutamani kujua chanzo cha kuvunjika ndoa yao ni kipi, kutokana wawili hao wamekaa kwa muda wa mchache kwenye ndoa hiyo kwa takribani miezi mitano huku akijitetea kuwa hajawahi kumuacha mke wake japo walikuwa na migogoro mingi ndani ya nyuma yao.
"Sijaachana na mke wangu Nawal kwa sababu bado sijatoa talaka mpaka muda huu kusema simtaki aendelee na maisha yake, japo kulikuwepo na msuguano wa hapa na pale ambao naamini haukuwa unatokana baina yetu, bali ulikuwa unataka na famili yake", alisema Nuh Mziwanda.
Pamoja na hayo, Nuh aliendelea kwa kusema "Nawal hajawahi kuniambia mimi na yeye basi tuachane, ila ninavyokumbuka alinipigia simu siku chache kabla ya kuolewa akitaka talaka yake wakati yupo nyumbani kwa wazazi wake. Maana alikuwa anapenda sana maamuzi ya kukimbilia kwao kila tunapopishana kwa hata jambo ndogo pamoja na kutaka talaka sasa sijui kwa sababu jamaa aliyemuoa ana uwezo wa kifedha kwamba anaweza akazungusha 'mkwanja' pale 'home' kwao", alisema Nuh Mziwanda.
Kwa upande mwingine, Nuh Mziwanda alisema aliamua kubadili dini yake na kuingia katika uislamu ni kutokana na kuwa alimpenda sana Nawal kwa kuwa ni mwanamke pekee aliyeweza kubeba ujauzito kati ya wanawake wote aliyokuwa nao kabla ya kufunga naye ndoa kwa mara ya kwanza.