SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 15 Agosti 2017

T media news

RC Dodoma Amevunja Mabaraza ya Biashara

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jodarn Rugimbana amevunja mabaraza ya biashara mkoani hapa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumika kisiasa.

Akizungumza leo Jumanne ofisini kwake, Rugimbana amesema mabaraza yaliyovunjwa ni ya wilaya na la mkoa.

Amewaagiza wakuu wa wilaya kusimamia uundwaji wa mabaraza hayo ndani ya siku saba.

Amesema mabaraza yatakayoundwa yalenge kutatua changamoto zilizokuwa zikiyakabili.

Pia amesema mabaraza hayo anataka yasimamie uanzishwaji wa viwanda.