SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 1 Julai 2017

T media news

Exclusive: Ally Yanga mpya ameibukia Ndondo Cup

Baada ya Ally Yanga kufariki, kuna jamaa ameibuka na kuamua kubeba jukumu la kuvaa uhusika wa Ally Yanga, Mark Yanga ameonekana kwenye mechi ya Ndondo Cup akiwa katika mwonekano tuliozoea kuuona kwa Ally Yanga enze za uhai wake wakati  alipokuwa akiishangilia Yanga na timu za taifa.

Dauda TV ilipata fursa ya kupiga story na Mark Yanga ambaye ameeleza sababu za yeye kuamua kuvaa viatu vya Ally Yanga lakini pia ameomba wana Yanga wampe ushirikiano ili aweze kuliziba pengo la kipenzi chao Ally Yanga.

Swali kubwa linaloulizwa ni kwamba, Mark Yanga atatosha kwenye viatu alivyokuwa akivivaa  Ally Yanga?