SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 12 Juni 2017

T media news

Ukweli Mchungu...Mikataba Inasainiwa "Gizani", Ripoti Inakabidhiwa Hadharani! Tuendelee Kushangilia..!!!?



Kuna mambo yanatafakarisha sana. Na hili ni miongoni mwa mambo hayo! Leo ripoti ya pili ya "wataalamu" (wanasheria na wachumi) inakabidhiwa kwa Rais. Tangu juzi kumekuwa na hamasa kubwa mitandaoni ya kututaka wananchi leo tukae mbele ya tv kutazama tukuo hilo. 

Kuna tuswali twa kujiuliza:

1. Kama mikataba ya madini tuliyoingia ilisainiwa "gizani" kwanini ripoti iliyochunguza mikataba hiyo hiyo inakabidhiwa hadharani huku vyombo vyote vya habari vikitakiwa kusitisha shughuli zingine na kuhamia kwenye tukio hilo?

2. Kama kuna vipengele vya kisheria vinavyotaka kuwepo kwa "usiri" kwenye mikataba hiyo (kama ambavyo huwa tunaambiwa [wanasheria wanaweza kunisaidia hapa]) hiki kinachofanywa sasa hakina athari yeyote kisheria?

3. Hao wanaotaka ripoti hizo zikabidhiwe hadharani lengo lao ni nini hasa?

4. Je, ni sawa na ina tija kwetu wanyonge kiasi cha kushangilia mno, ripoti ya uchunguzi kuhusiana na mikataba ya ACACIA kukabidhiwa hadharani, lakini mikataba ya ununuzi wa bombadier; na mengine kufanyika gizani?

Na mimi pia ni mzalendo!

Chanzo JF